Matthew 8:19-22

19 aKisha mwalimu mmoja wa sheria akamjia Isa na kumwambia, “Mwalimu, nitakufuata kokote uendako.”

20 bNaye Isa akamjibu, “Mbweha wana mapango, nao ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana mahali pa kulaza kichwa chake.”

21 cMwanafunzi mwingine akamwambia, “Bwana, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.”

22 dLakini Isa akamwambia, “Nifuate, uwaache wafu wawazike wafu wao.”

Isa Atuliza Dhoruba

(Marko 4:35-41; Luka 8:22-25)

Copyright information for SwhKC